Include this script into your page along with the iframe for a responsive media embed
Tangu jadi wachungaji na wahubiri na baadhi ya wanaojiita manabii wamekuwa wakidaiwa kufanya yale ambayo yameshindikana kufanyika kupitia sayansi ya kisasa. Yaani kuponya wagonjwa kwa kumshika kwa mkono, au kupigwa na upepo au kwa kutumia njia ya ajabu. Lakini ni wachache kama wapo ambao wanaponya kwa imani. Katika miezi michache iliyopita maelfu ya watu wa matabaka tofauti wanamiminika katika kijiji kimoja kaskazini mwa Tanzania ili kupata kikombe cha dawa kutoka kwa aliyekuwa mchungaji wa Kanisa la Lutheran, Ambilikile Mwasapile. Mzee huyo wa umri wa miaka 72 anasema kuwa anaweza kutibu magonjwa sugu kama ukimwi, saratani na hata kisukari. John-Allan Namu ambaye amerejea ameandaa sehemu ya kwanza ya makala yafuatayo ya maajabu loliondo ambayo yamesomwa na Rashid Abdallah. www.ntv.co.ke