Stamina Ft Jux - Alisema (BONGO HIP HOP)

 • studio snap records,producer kevy,dogo anapunch lines za ukweli
  INTRO; IS moro town beib,YOU know what kevy?this is so conscious men
  Vers 1; Stamina
  Sio kila mchaga muuza duka,so nisiogope kuitwa mangi
  Kupanda na kushuka,ndio chart isiyohitaji rangi
  Bora kuitwa mshamba,kwenye group la matapeli
  Subira ikikosa kamba,nijipange kuivuta heri
  Alisema nisilete uchizi,mbele ya daktari wa akili
  Nisiwe na hasira za mkizi,ili mvuvi anifanye dili
  Kukosa na kupata,ndio mechi isiyokua na draw
  Kama maisha karata,mchangaji nimkabe koo{ooooh}
  Madawa ya kulevya,niogope yatanipa uchizi
  Maishani nisiwe dereva,kwenye basi la wazinzi
  Kengeza ndo macho yangu,nisimcheke mwenye chongo
  Nipendezeshe maisha yangu,kama dressing table ya mkongo
  Nisile ada kisa demu,mapenzi hayana mradi
  Maisha ni ps game, hayachezeki bila pad
  Elimu ya mtaani,niijue ili nikuze ukoo
  Ila elimu ya darasani,nisihitimu bila ya joh{alisema}
  Chorus; Jux
  Nifanye nachofanya bwana mimi nisizubae,uwezo ninao{alisema}
  Maneno yakisemwa wala mimi nisishangae,niachane nayo{alisema}
  Ubinadamu kazi{alisema},nisiwe na haraka na maisha{alisema}
  Nisichague kazi{alisema}nakumbuka ieeeiiiiiiii
  Vers 2; Stamina
  Usoni nisipretend ugumu,wakati moyoni nina usharo
  Ugangstar sio kuvuta ndumu,nijipange nitafuta mipalo
  Kama pesa hazilali,mtafutaji nisichonge kitanda
  Asali ikiwa juu ya dali,mlinaji nisichome kibanda
  Alisema mjini mipango,sio urefu wa magorofa
  Samaki akiliwa na chambo,nijue mvuvi ameshaanza urofa
  Nisinywe gongo na biskuti,nikadhani ndio janja ya teja
  Nikaze buti ili nijibust,wapinzani wasiniite kinega
  Kama muda ni pesa,nifungue account ya saa
  Nisiseme boom linatesa,huku principle anashinda bar
  Maisha trailer za kanumba,nisiogope kufa kiuongo
  Mimba ya ujinga haina mkunga,nitafute ujanja kwa usongo
  Nisimdharau fukara,kisa nimemzidi kipato
  Mtoto nisimfanyie tohara,akikua aniite pilato
  Fisadi akiwa jogoo,tetea nitafute kambi
  Mziki una kwashiorkor,nisiache hadi unipe kitambi{alisema}
  Chorus; Jux
  Nifanye nachofanya bwana mimi nisizubae,uwezo ninao{alisema}
  Maneno yakisemwa wala mimi nisishangae,niachane nayo{alisema}
  Ubinadamu kazi{alisema},nisiwe na haraka na maisha{alisema}
  Nisichague kazi{alisema}nakumbuka ieeeiiiiiiii
  Vers 3; Stamina
  Nisishangae kukuta bwanga,kwenye chumba cha mamodel
  Ila nishangae kuziona shanga,kwenye kiuno cha mtoto mdogo
  Kipimo cha utapeli,hakipimwi na mzani wa ubongo
  Nisibishane na ukweli,ikiwa nina chembe za uongo
  Mfupi ndio aliyegundua ngazi,ilimradi apate virefu
  Nisimtukane mzazi,nitapata radhi ya ukosefu
  Selemara arudi veta,mende akiangusha kabati
  Na daudi akipigwa ngeta,nijue kesi kwa goliati
  Primary na shule ya msingi,zina utofauti wa kimasilahi
  Inabidi nione vifo vingi,ili nijue thamani ya uhai
  Nguvu za uongo wa video,zisinipotezee ujana
  Nisijiite jembe huku kimeo,wakati pabichi nakwama
  Nikikosa fasta nitubu,masizi yasigeuke kiwi
  Na nisiogope kuitwa bubu,kwenye kundi la viziwi
  Nisiforce penzi kwa changu,ni bora nikatumia detto
  Na moro ndio mkoa wangu,nikiukana wataniita petro{alisema}
  Chorus; Jux
  Nifanye nachofanya bwana mimi nisizubae,uwezo ninao{alisema}
  Maneno yakisemwa wala mimi nisishangae,niachane nayo{alisema}
  Ubinadamu kazi{alisema},nisiwe na haraka na maisha{alisema}
  Nisichague kazi{alisema}nakumbuka ieeeiiiiiiii
  Bridge;jux
  Uwezo ninao{alisema}
  Niachane nao{alisema}
  Ontro; Stamina
  Kama mungu alitoa,tusishangae anapo twaa
  Amini kila binadamu alizaliwa shujaa
  So this one,is dedicated to all who lost their beloved ones

  Category : Bongo Flava (mp3)

  #Stamina#Jux#Alisema#snap#records#kevy

  0 Comments and 0 replies
arrow_drop_up