Loading the player...

Fid Q feat Barakah The Prince - MAFANIKIO (OFFICIAL LYRIC VIDEO)

 • intro: Barakah The Prince
  kila mtu anataka mafanikio..
  verse 1:Fid Q
  Kujisikia nipo juu mie sitaki hizo deals/
  sipendi makuu hivyo nitabaki kuwa real../
  a kila track ya Q aaah,.. ni wazi utaifeel/
  i wazi iko full aah MZAZI ninakill/
  inamwagika kama Masika../ ninaheshimika na sio kanjibai/
  kwa huu mziki wa bajaji hadi kwa washkaji wenye macadillac/
  unawashika ile kibabylon.. unauzika sana maghetoni/
  ilimradi tu wawe happy more..midadi tu ila party noooo/
  mkisinzia mtaniudhi nishawapa vyeo/
  tuwape wapuuzi waliodai hii haiuzi haya matokeo/
  safari ni hatua.. kufika inabidi uianze/
  haina kukita au kusita.. inabidi ukaze/
  ingia, ongoza au fuata mkia, kukimbia ni mwiko/
  kuanzia ulipo sio sawa na kubakia ulipo/
  ikisema 'chini hapana' nina maana fanya unyanyuke/
  a ukiamini umesimama mwana.. komaa usianguke/
  ukijituma na neema inakaribia../
  yuma walio-give up mapema wangekaza wangeifikia/
  penye... happy.. jitusu.. unafki usiuruhusu/
  yajue ya kuzingatia ili uachane na yasiyokuhusu/
  kibongobongo longolongo shazi/
  endelea kusaka mchongo hata ukipata kazi/
  HOOK: Barakah the prince
  Tunachukiana? ndio../
  ila sio sababu kuacha riadha ya mafanikio/
  ongeza mbio/
  sababu kila mtu, kila kona anasaka mafanikio/
  haukungoji wakati.. ooh wewe/
  zinapita nyakati..ooh wewe/
  muda wako bahati.. oh wewe/
  verse 2:Fid Q
  Na kughairisha kisa haupati sapoti/
  i kujificha na kuuliza giza.. iko wapi ile tochi?/
  haupati ile noti/
  a wakati wa ule uboss ushapotea/
  hautaki ukose? usiache ofcoz endelea/
  utafanikiwa kwa unachojua au unachofanya/
  wachache ndio hutusua kwa jinsi tu wanavyoonekana/
  mafanikio hayaji ukikata tamaa../
  yenyewe huwafuata wanaojituma na wale wasiosukumwa na njaa/
  sipigi kila dili mipaka imezingatiwa/
  sitaki kuwa tajiri ninataka kufanikiwa/
  ili kuheshimiwa kwanza ni lazima ujiheshimu/
  lakini kufanikiwa ni maujanja tu sio lazima elimu/
  ili kuyadaka wengine hugeuka wabaya/
  mafanikio kwenye kuyasaka wengine hugeuka malaya/
  hugeuka was(i)o haya/
  kutwa utawakuta kwa babu/
  a anayefanya mambo ya maana huwa hana muda wa kuyahesabu/
  kwenye kuyasaka hakikisha haufilisiki/
  haupotezi maisha au vile vitu havinunuliki/
  sio kama hatucheki kwasababu tumezeeka?/
  ope.. ni tunazeeka kwasababu hatujawahi cheka/
  HOOK: Barakah the prince
  Tunachukiana? ndio../
  ila sio sababu kuacha riadha ya mafanikio/
  ongeza mbio/
  sababu kila mtu, kila kona anasaka mafanikio/
  haukungoji wakati.. ooh wewe/
  zinapita nyakati..ooh wewe/
  muda wako bahati.. oh wewe/
  utumie basi... eeeh eeeh/
  bridge: Barakah The Prince
  una mpenzi (na) uko lonely?/
  im sorry ndugu.. haujafanikiwa/
  maisha ni kama boli, magoli ndio kufanikiwa/
  oooh ooh oooh..oooh.. ndio kufanikiwa/
  kila mtu anataka mafanikio.../
  outro:Barakah The Prince
  hhhmmm.. hhhhmmm.. oh mafanikio
  oh mafanikio
  kila mtu anataka mafanikio

  Category : Bongo Flava Videos

  #Fid Q#Barakah The Prince#MAFANIKIO#Bongo Flava

  0 Comments and 0 replies
arrow_drop_up