Include this script into your page along with the iframe for a responsive media embed
Mbunge wa Singida Mjini nchini Tanzania, Tundu Lissu ambaye yuko kwenye ziara ya vyombo vya habari mbalimbali duniani, amemfunika vibaya kwa hoja Balozi wa Tanzania nchini Marekani, Wilson Masilingi walipokutana uso kwa uso kwenye kipindi cha Straight Talk Africa kinachoendeshwa na Shaka Ssali wa Voice of America mjini Washington, DC. Katika kipindi hicho ambacho kilikuwa kinazungumzia Uhuru wa Kujieleza katika mataifa mbalimbali ya Africa pia kilimjumuisha mwanamuziki wa Uganda ambaye pia ni mwanaharakati na mbunge, Bobi Wine. Tundu Lissu ambaye alinusurika jaribio la kutaka kuuawa baada ya kupigwa risasi 16 mwilini katika mji mkuu wa Tanzania, Dodoma. Mpaka hivi sasa, Tundu Lissu ameshafanyiwa upasuaji mara 22. Originally posted at www.voanews.com/a/4775553.html