Loading the player...

Kamanda wa Polisi Arusha Jonathan Shana Akihutubia Mkutano wa CCM

  • Kamanda wa Jeshi la Polisi Polisi Mkoa wa Arusha, Jonathan Shana anadaiwa kugeuka mwanasiasa na kada wa CCM huku akisahau majukumu yake baada kuhutubia Mkutano wa ccm jijini Arusha na kuwataka wanaccm watembee kifua mbele kwa sababu jeshi la Polisi ni lao na litawalinda kwa ushindi wowote.
    RPC Shana amekuwa akipewa nafasi ya kuhutumia kwenye mikutano ya ccm na kujikuta akiweka pembeni Kazi yake aliyoajiriwa nayo jambo ambalo baadhi ya wakazi Arusha wamemtaka IGP kumtafutia Kazi nyingine kwakuwa ameonyesha uwezo wake ni mwanasiasa na si mtendaji.
    Akihutubia katika ukumbi wa mikutano wa Simba Holl (Aicc) jijini Arusha Shana aliwaambia wanaccm kwamba yeye ni mwanasheria na mwanasiasa mzoefu anayetumikia ilani ya chama hicho na kuwataka wanaccm washikamane kwakuwa wanalindwa na jeshi lake usiku na mchana.
    Huu ni ukiukwaji mkubwa wa maadili yake ya kazi na ingekuwa yuko kwenye nchi yeyote inayofuata sheria, haki na utawala bora, kamanda huyu wa Polisi muda huu angekuwa ameshafukuzwa kazi mara moja. Pamoja na kudai amesoma sheria, kamanda huyu bado anaonekana ni mbumbumbu na goigoi wa sheria.

    Category : News & Politics

    #Jonathan Shana#Kamishna Msaidizi Polisi#Kamanda Polisi Arusha#CCM#Kada

    0 Comments and 0 replies
arrow_drop_up